Kaizari

Pitio kulingana na tarehe 20:56, 20 Septemba 2006 na Kipala (majadiliano | michango) (viungo vya miaka na masahihisho)

Kaisari ni cheo cha mfalme mkuu. Asili ya jina ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina lilikuwa cheo.

Cheo cha Kaisari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki (Bizanti) hadi 1453. Katika Ulaya yenyewe mfalme wa Wafranki Karolo Mkuu alipokea cheo cha "Caesar" au Kaisari. Baadaye wafalme Wajerumani waliomfuata Karolo Mkuu katika sehemu ya mashariki ya ufalme wake waliendelea kutumia cheo hiki cha Caesar au Kaisari.

Neno la Kaisari liliingia katika lugha ya Kiswahili wakati wa ukoloni wa Kijerumani huko Tanzania. Austria na Ujerumani zilitawaliwa hadi mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia 1918 na wafalme wenye cheo cha "Kaisari" (kijer.: Kaiser). Vilevile mfalme wa Urusi alikuwa na cheo kilekile kilichoitwa "Tsar" kwa Kirusi, ilhali neno hili limeundwa pia kutoka kwa "Caesar".

Lugha za Kiingerezea na Kifaransa zilitumia cheo tofauti cha Macaesar wa Kiroma ndicho "Imperator" (=mwenye amri, mwenye mamlaka, jemadari)kilichokuwa "Emperor" (Kiing.) au "Empereur" (Kifaransa).

Kaisari ni cheo cha mfalme aliye juu ya wafalme wengine. Kutokana na uzuefu huu hata Shah wa Uajemi, mtwala wa Japani na Negus Negesti wa Ethiopia wanaweza kutajwa kwa cheo cha "Kaisari".