Ng'ombe
Ng'ombe | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kundi la ng'ombe
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Nususpishi 5:
|
Kwa kundinyota inayoweza kuitwa Ng'ombe angalia hapa Tauri (kundinyota)
Ng'ombe (zamani pia bakari) ni wanyama wakubwa wanaokula nyasi. Ni wanyama wanaofugwa kwa wingi sana kwa ajili ya nyama, maziwa, ngozi au pia kwa kuvuta plau au gari la kukokotwa.
Kibiolojia ni wanyama wa jenasi Bos. “Ng'ombe-kaya” ni aina zifugwazo za “ng'ombe-mwitu” (Bos primigenius).
Kwa asili kuna aina mbili za ng'ombe-kaya: ng'ombe wa Ulaya na ng'ombe wa Uhindi ambazo ni nususpishi za B. primigenius (B. p. taurus na B. p. indicus mtawalia, ingawa mara nyingi nususpishi hizo zinaainishwa kama spishi za B. taurus na B. indicus). Zinatoka kwa nususpishi za zamani B. p. primigenius na B. p. namadicus.
Siku hizi ni vigumu kufahamu nususpishi za ng'ombe, kwa sababu takriban aina zote za ng'ombe ni chotara sasa.
Ng'ombe hula nyasi na hutembea kwa kwato. Ng'ombe waliofugwa na binadamu walitokana na ng'ombe-mwitu ili kujipatia nyama na maziwa. Katika nchi nyingi hutumiwa pia kama mnyama wa mizigo anayevuta plau au magari.
Wataalamu huamini ya kwamba aina zote za ng'ombe zina asili katika Mashariki ya Kati mnamo milenia ya 9 KK ambako watu waliwahi kuwafuga na kutoka hapa ufugaji ng'ombe ulisambaa kote duniani.
Ng'ombe wanapatikana kote duniani na kuna aina kwa kila namna ya hali ya hewa. Wengine huishi katika milima baridi ya Uskoti na Skandinavia, wengine katika joto la Afrika au Australia.
Wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.
Nususpishi
- Bos primigenius, Ng'ombe
- †Bos p. africanus, Ng'ombe-mwitu wa Afrika – imekwisha sasa
- Bos p. indicus, Ng'ombe wa Uhindi
- †Bos n. africanus, Ngombe za kinigeria, Zebu
- †Bos p. namadicus, Ng'ombe-mwitu wa Uhindi – imekwisha sasa
- †Bos p. primigenius, Ng'ombe-mwitu – imekwisha sasa
- Bos p. taurus, Ng'ombe wa Ulaya (Cattle)
Picha
Viungo vya Nje
- Cattle Breeds website - Oklahoma State University
- Ufugaji na magonjwa ya Ng'ombe - Sekta ya Mifugo Tanzania
- PBS Nature: Holy Cow (about cows in general)
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ng'ombe kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.