Motokaa : Tofauti kati ya masahihisho
Content deleted Content added
d Bot: Migrating 132 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q1420 (translate me) |
Link suggestions feature: 3 links added. |
||
(marekebisho 28 ya kati na watumizi wengine 15 na yule ambaye hajaonyeshwa) | |||
Mstari 1:
[[Picha:Ford.mondeo.mk3-black.front-by.ranger.jpg|thumb|'''Ford Mondeo''' ni motokaa ndogo ya kubeba abiria wachache, kwa mfano [[familia]] ndogo.]]
[[Picha:WA SES Toyota Landcruiser.jpg|thumb
'''Motokaa''' (kutoka [[Kiingereza]] "motor car"<ref>
Kuna aina nyingi za motokaa
Mengine ya kubeba abiria ni [[Basi|mabasi]] ambayo ni pia aina ya motokaa lakini mara nyingi hutajwa kama [[kundi]] la pekee, sawa na [[Lori|malori]] ambayo ni motokaa kubwa za kubeba [[mizigo]]. Kuna kila aina ya mchanganyiko kati ya aina hizi.
[[Picha:Chassis with suspension and exhaust system.jpg|thumb||Fremu ya motokaa pamoja na magurudumu, bila injini wala bodi.]]
== Muundo ==
Motokaa huwa na [[injini]] (mota) inayosukuma [[magurudumu]] kupitia [[giaboksi]]. Injini pamoja na magurudumu na bodi hushikwa na
Dereva hutumia mitambo ya kutawala motokaa ambayo ni hasa:
Mstari 19:
Mitambo ya lazima kwa usalama wa gari ni taa zake za nje mbele na nyuma, kiashirio au indiketa ya kuonyesha nia ya kubadilisha mwelekeo, kifuto au waipa inayosafisha kioo cha mbele wakati wa mvua.
Magari ya kisasa huwa na mitambo mengi mengine kama redio, vyombo vya muziki, kiyoyozi, siku hizi pia kompyuta ndogo ya kusimamisha injini au kuonyesha [[ramani]] ya njia pamoja na kutoa maelezo kuhusu njia kwa dereva kwa kutumia sauti iliyorekodiwa.
Injini kwa kawaida hupata nguvu yake kwa kuchoma [[petroli]], [[diseli]] au gesi. Motokaa za kwanza zilitumia pia nguvu ya mvuke. Motokaa za kisasa kabisa zinatumia pia injini ya umeme.
== Historia ya motokaa ==
Kwa karne nyingi watu walitumia magari yaliyovutwa na wanyama kwa mfano [[farasi]], [[punda]] au
=== Injini za mvuke ===
Baada ya kugunduliwa kwa [[injini ya mvuke]] nguvu yake ilitumiwa pia kwa [[Chombo cha usafiri|vyombo vya usafiri]]. Kutokana na uzito wa injini pamoja na magari yaliyoweza kuvumilia uzito mkubwa wa injini pamoja na maji na kuni iliyohitajika kuchemsha maji vyombo hivi havikufaa barabara za kawaida vikatumia njia ya [[reli]] za chuma. Nusu ya pili ya karne ya 19 iliona maendeleao ya kutengenezwa kwa motokaa za mvuke madogo yaliyotembea barabara za kawaida katika nchi za Ulaya na Marekani.
=== Injini za umeme ===
Sehemu ya pili ya karne ya 19 iliona pia magari yaliyoendeshwa kwa nguvu ya umeme. Magari haya yana faida nyingi; muundo wa gari ni rahisi zaidi kwa sababu haihitaji giaboksi wala gia na gari halina makelele pia hautoi
[[Picha:Sfrancisco trolley.jpg|thumb
Mwaka 1900 asilimia 40 za motokaa zote nchini Marekani zilikuwa na injini za mvuke, 38 % za umeme na 22% za petroli. Mjini [[New York (jimbo)|New York]] nusu ya motokaa zote zilikuwa na injini ya umeme.
Baadaye magari ya petroli yalisogea mbele kwa sababu yaliweza kutembea mbali kwa kujaza mafuta kuliko
Katika nchi kadhaa mabasi ya umeme yameendelea kutumiwa katika miji mikubwa
Katika karne ya 21 teknolojia ya beteri ilisogea mbele kutokana na upanuzi wa matumzi ya simu za mkononi. Beteri ziliendelea kuwa ndogo zaidi na pia kushika umeme kwa muda mrefu zaidi. Maendeleo haya yametumiwa kwa kubuni motokaa mpya za umeme. (tazama chini)
=== Injini za mwako ndani (petroli na diseli) ===
[[Picha:1885Benz.jpg|thumb|Motokaa ya kwanza ya Benz ya 1885]]
Katika karne ya 19 wahandisi mbalimbali walianza kutengeneza injini za mwako wa ndani zilizochoma gesi au petroli ndani yake. Injini ya kwanza iliyofaulu kuanzia [[1876]] na kutengenezwa kwa wingi ilikuwa ni ile ya Mjerumani
Maendeleo ya motokaa zilizotumia injini mwako ndani yalikuwa haraka. Mwanzoni yalikuwa na matatizo mengi hasa uhaba wa petroli. Benz alinunua mafuta kwa gari lake kwenye duka la dawa.
Mwaka 1892 mhandisi Mjerumani
[[Picha:1926 Ford Model T Tudor Sedan FLA915.jpg|thumb
== Ushindi wa motokaa ==
Mwanzoni motokaa zilikuwa ghali sana zikanunuliwa na matajiri pekee. Mwaka 1914 mhandisi wa [[Marikani]] [[Henry Ford]] alianza kutengeneza gari lake la "Ford Model T" kiwandani akitumia mbinu mpya; aligawa matengenezo ya gari kwa hatua mbalimbali zilizotekelezwa na wafanyakazi walioshughulika hatua moja-moja tu. Mbinu huu ulisababisha utekelezaji wa haraka kwa sababu kila mfanyakazi alikuwa na shughuli chache zu alizojua kwa undani kabisa akiwa na vifaa na vipuri vyote pale alipofanya kazi bila kupotezy muda. Kwa njia hii Ford aliweza kutengeneza magari mengi tena kwa bei nafuu na hata watu wenye mapato ya wastani waliweza kununua gari hili. Mfanyakazi wa Ford aliweza kununua gari kwa mshahara wa miezi minne. Kwa jumla magari milioni 15 ya Ford T yalitengenezwa hadi 1927.
Line 56 ⟶ 58:
== Mielekeo mipya ==
Tangu miaka ya 1970 kuzidi kwa motokaa kulileta pia matizo mapya:
* machafuko kwa mazingira kwa kelele na hewa chafu ya eksozi. Machafuko haya yalionekana kusababisha magonjwa kama kansa pia kuleta uharibifu kwa machafuko kwa hewa. Matokeo yake yalikuwa
* kupanda kwa bei ya petroli tangu
* hofu ya kuishi kwa mafuta ya petroli baada ya
Jibu la wahandisi lilikuwa majaribio ya kuboresha injini zisizotumia mafuta. Ni hasa teknolojia mbili zilizoendelea kushughulikiwa:
Line 64 ⟶ 66:
* injini ya umeme
Kwa jumla magari ya umeme bado hutegemea mbinu za kubeba nishati njiani kwa beteri. Siku hizi ni hasa injini za umeme zinazopokea jitihada nyingi. Tatizo hadi leo ni uzito, uwezo na gharama za
Mwelekeo tofauti ni majaribio ya kutengeneza umeme njiani. Hapa kuna njia mbili hasa:
*
* hasa makampuni ya Japani yameshafaulu kutoa na kuuza magari chotara yanaounganisha injini ya umeme na injini ya petroli. Gari linaanza safari kwa nguvu ya beteri; beteri ikikwisha injini ya mafuta inawaka na kujaza
== Ya kuangazia unaponunua motokaa ==
Haya ndiyo mambo ya kuangazi kabla ya kununua gari lako likiwa jipya au hata la zamani.
===Usiwe na pupa===
<references/>▼
Usiwe mwenye pupa wa kununua gari kabla ya kufanya utafiti ili ulijue gari lile zuri kabisa na ambalo litadumu kwa muda mrefu. Ukifanya utafiti wako kwa mitandao, kwa vitabu au marafiki walio na lile gari, basi utafanya uamuzi mwema wenye busara.
===Jaribu kuliendesha gari===
Ni vizuri uliendeshe gari kabla ya kulinunua. Hili huitwa kwa Kiingereza "test drive" na muuzaji atakuruhusu kufanya hivi
===Kuwa na makanika wako===
Huenda ukalinunua gari lililozeeka na kwa maana wewe ni mgeni katika kununua magari, ni vizuri uliangalie na makanika ambaye atakupa mashauri.
===Nunua gari utakalomudu===
Ni vizuri uangalie gari ambalo wewe mwenyewe utalimudu, isiwe kwamba ni gari linalohitaji mambo mengi yatakayokushinda.
===Angalia bima ya gari===
Gharama ya bima ni jambo lingine la kuangazia unaponunua gari.
===Nambari ya usajili===
Serikali zahitaji kwamba kila gari liwe na nambari ya usajili. Nambari hii pia yaweza kukusaidia kujua umri wa gari.
==Tanbihi==
== Viungo vya nje ==
{{commons|Automobile}}
* [http://www.automuseum-dr-carl-benz.de de:
* [http://www.bertha-benz.de/indexen.php?inhalt=home en:
* [http://l3d.cs.colorado.edu/systems/agentsheets/New-Vista/automobile Historia ya motokaa toka Chuo Kikuu cha Colorado] {{Wayback|url=http://l3d.cs.colorado.edu/systems/agentsheets/New-Vista/automobile |date=20180622022111 }}
* [https://www.wired.com/2012/02/autonomous-vehicle-history Historia ya magari yanayojiendesha yenyewe bila dereva]
* [https://www.wikihow.com/Take-Care-of-Your-Own-Car Jinsi ya kutunza gari lako]
* [https://auto.howstuffworks.com/flying-car.htm Kuhusu magari yanayoruka]
{{tech-stub}}
[[Jamii:Motokaa]]
|